BANDORA AUNGANA NA VIONGOZI KATIKA UZINDUZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA | BUTONDO DIGITAL

Monday, November 2, 2026

BANDORA AUNGANA NA VIONGOZI KATIKA UZINDUZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA

  Suzy Butondo       Monday, November 2, 2026

 


Diwani wa Kata ya Chemchem, Manispaa ya Tabora, Bandora Salum Mirambo, yupo jijini Dodoma kushiriki katika uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba.

Uzinduzi huo umefanyika  jijini Dodoma, ukiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba ni hatua muhimu katika kuimarisha utendaji wa Serikali, kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuimarisha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma.

Mji wa Serikali Mtumba Alama ya maendeleo na mageuzi katika utendaji wa Serikali.

logoblog
Previous
« Prev Post