TSIA YATAKA SHERIA YA ULINZI BINAFSI IHARAKISHWE | BUTONDO DIGITAL

Tuesday, October 27, 2026

TSIA YATAKA SHERIA YA ULINZI BINAFSI IHARAKISHWE

  Suzy Butondo       Tuesday, October 27, 2026

 


Mkutano mkuu wa 18 wa kazi wa chama cha sekta binafsi ya ulinzi Tanzania TSIA umefanyika jijini Dodoma ukiangazia changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa sheria inayosimamia sekta hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha sekta binafsi ya ulinzi Tanzania kanda ya kati Bandora Salum Mirambo amesema katika mkutano huo wamewasilisha changamoto kadhaa ikiwemo ucheleweshaji wa utoaji wa vibali vya umiliki wa silaha.

Bandora amesema licha ya kukua kwa sekta hiyo bado wana changamoto ya Ukosefu wa sheria inayosimamia sekta hiyo wakiiomba serikali kuharakisha mchakato wa kutungwa kwa sheria maalum ya kusimamia makampuni na sekta binafsi ya ulinzi nchini ili kuweka miongozo na usimamizi bora.

Mkutano huo umehudhuriwa na naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Daniel  Sillo ambae ametoa mwelekeo wa changamoto zilizowasilishwa akisema wanafahamu umuhimu wa kutungwa sheria ya usimamizi wa sekta binafsi ya ulinzi na mamlaka zinazohusika ziendelee kufanya mashauriano na TSIA ili maoni yote yazingatiwe katika utungwaji wa sheria hiyo.

Sillo amesema sekta binafsi ya ulinzi imekua na mchango mkubwa katika kutoa ajira, kuimarisha ustawi wa jamii, kulinda mali na watu na Kusaidia taasisi mbalimbali kufanya kazi katika mazingira salama.

logoblog
Previous
« Prev Post