ABIRIA 54 WANUSURIKA KIFO, BASI LA ABOOD LATEKETEA KWA MOTO KAHAMA | BUTONDO DIGITAL

Friday, November 13, 2026

ABIRIA 54 WANUSURIKA KIFO, BASI LA ABOOD LATEKETEA KWA MOTO KAHAMA

  Suzy Butondo       Friday, November 13, 2026

 



Na Suzy Butondo 

SHINYANGA
Abiria 54 waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kagera wamenusurika kifo baada ya basi mali ya Kampuni ya Abood, lenye namba za usajili T 285 EAV, kuteketea kwa moto katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku tukio hilo likisababisha hofu kubwa kwa abiria waliokuwa ndani ya basi hilo, ambao kwa bahati nzuri wamefanikiwa kuokoa maisha yao.

Ni alfajiri ambayo haitasahaulika kwa abiria hao, ambao walikuwa na matarajio ya kufika salama katika safari yao, lakini ghafla walijikuta wakikabiliwa na tukio la kutisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kushika moto.

Pamoja na kunusurika kwa abiria hao, baadhi ya mizigo yao imeteketea kwa moto, hali iliyowaacha katika simanzi na majonzi kutokana na kupoteza mali zao.

Baadhi ya manusura wa tukio hilo ni Joseph Matabaro, Betrice Baitwa na Nzambakiza Ndamuru, ambao wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea na jinsi walivyofanikiwa kunusurika katika ajali hiyo.
logoblog
Previous
« Prev Post