SAID NKUBA ASIFIWA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAMA NA SERIKALI | BUTONDO DIGITAL

Thursday, August 6, 2026

SAID NKUBA ASIFIWA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAMA NA SERIKALI

  Suzy Butondo       Thursday, August 6, 2026

 I

 Diwani wa Kata ya Chemchem, Bandora Salum Mirambo, amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Said Nkumba, kwa uongozi wake wenye kuimarisha ushirikiano kati ya chama na serikali, hali iliyochangia kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Akizungumza, Bandora amesema kuwa Nkumba ameendelea kusimamia, kufuatilia na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali, hatua inayosaidia kuhakikisha ahadi zilizotolewa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM zinatekelezwa kwa ufanisi.

Aidha, amempongeza Mwenyekiti huyo kwa juhudi zake za kuimarisha chama, kuendeleza uenezi wa itikadi na sera za CCM, pamoja na kuhakikisha maamuzi ya vikao vya juu vya chama na yale ya ngazi ya mkoa yanatekelezwa kwa vitendo.

Bandora amesema uongozi wa aina hiyo unaendelea kuimarisha mshikamano ndani ya chama na kuongeza imani ya wananchi katika utekelezaji wa agenda za maendeleo.

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE.

logoblog
Previous
« Prev Post