TULILIA TULIPOMPOTEZA KAMANDA ABWAO, TUENDELEE KUMUOMBEA KWA NAMNA TUNAVYOWEZA – DIWANI BANDORA | BUTONDO DIGITAL

Wednesday, July 29, 2026

TULILIA TULIPOMPOTEZA KAMANDA ABWAO, TUENDELEE KUMUOMBEA KWA NAMNA TUNAVYOWEZA – DIWANI BANDORA

  Suzy Butondo       Wednesday, July 29, 2026

 

Diwani wa Kata ya Chemchem, Bandora Salum Mirambo, amewataka wananchi kuendelea kumuombea aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao, huku wakielekea kumbukizi ya siku 40 tangu alipofariki dunia.

Bandora amesema kuwa licha ya kifo chake, Kamanda Abwao ataendelea kuishi katika mioyo ya wengi kutokana na utumishi wake na mchango alioutoa kwa jamii.

"Kamanda Abwao bado anaishi katika mioyo yetu. Kumbukumbu zake nzuri na mchango wake kwa jamii bado havijafutika. Tunapoelekea kumbukizi ya siku 40 zinazofanyika nyumbani kwake mkoani Morogoro, tuendelee kumkumbuka na kumuweka katika sala na dua zetu," amesema Bandora.

SACP Richard Abwao alifariki dunia tarehe Juni 20, 2026, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa za kifo chake ziliacha simanzi na huzuni kwa familia, ndugu, marafiki, watumishi wa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi waliomfahamu.

Kuelekea kumbukizi ya siku 40 tangu kifo chake, viongozi na wananchi wanaendelea kutoa salamu za pole na kuwaomba Watanzania kuendelea kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la milele.

"Tulilia tulipompoteza Kamanda Abwao tuendelee kumuombea kwa namna tunavyoweza ndugu yet u"amesema Bandora

Pumzika kwa amani, SACP Richard Abwao. Kumbukumbu zako zitaendelea kuishi mioyoni mwa wengi.

logoblog
Previous
« Prev Post