
Diwani wa Kata ya Chemchem, Manispaa ya Tabora, Bandora Salum Mirambo, ametoa pongezi za dhati kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, kufuatia kuaminiwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na kuteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Oganaizesheni, akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Issa Ussi Gavu.
Akizungumza kuhusu uteuzi huo, Bandora alisema:
"Nakutakia kila la heri Paul Chacha katika majukumu yako mapya. Nina imani utaendelea kulitumikia Chama kwa uzalendo, uadilifu na weledi kwa ajili ya kuimarisha misingi na maendeleo ya CCM."
Mbali na hilo, Bandora pia amempongeza Agrey Mwanri kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya John Mongella.
Paul Chacha na Agrey Mwanri wote wamewahi kulitumikia Taifa katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambapo walitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya mkoa huo.
Bandora amesema uteuzi wao ni ishara ya kutambuliwa kwa utendaji wao mzuri na amewatakia mafanikio katika majukumu yao mapya.
KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE. 🙏