ZAIDI YA NYUMBA 10 ZA ZINGIRWA NA MAJI SHINYANGA | BUTONDO DIGITAL

Wednesday, March 11, 2026

ZAIDI YA NYUMBA 10 ZA ZINGIRWA NA MAJI SHINYANGA

  Suzy Butondo       Wednesday, March 11, 2026

 uzy Butondo

Wakazi wa Mageuzi manispaa ya Shinyanga wakipita ndani ya maji



Na Suzy Butondo, Shinyanga

Zaidi ya nyumba kumi katika Mtaa wa Mageuzi Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga,zimezingirwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha, huku wananchi wa

kiomba Serikali kuwachimbia mitaro ili kuondoa adha wanayopata.

Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi wa Mtaa huo wamesema tatizo kubwa linalosababisha mafuriko hayo ni kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji, hali ambayo imekuwa ikichangia maji kukosa mwelekeo na hatimaye kuingia ndani ya nyumba zao.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mageuzi Doricas George na Emmanuel Shija wamesema baada ya kunyesha mvua hali imekuwa ngumu hasa kwa watoto wanaokwenda shule, ambao wamekuwa wakishindwa kuvuka mto na kushindwa kwenda shule na mvua zinaponyesha wakiwa shule wazazi hulazimika kuwafuata.

"Tunaiomba serikali itusaidie itengeneze barabara ili kuondokana na tatizo hili maana mvua kama hizi zikinyesha maji hukimbilia ndani, ambayo nihatari endapo ikinyesha wazazi watu wazima wakiwa hawapo"amesema Emmanuel.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mageuzi Vitalis Mugisha, amesema kuwa tatizo ni kubwa baada ya kukosekana miundombinu ya barabara ,ambapo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia ili waondokane na tatizo hilo.

Nae Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Pamphir, amesema kuwa hana taarifa kuhusu kuwepo kwa mafuriko katika Mtaa wa Mageuzi.







logoblog
Previous
« Prev Post