
Suzy Butondo,Shinyanga
Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amesema mradi wa upanuzi wa kituo cha kupooza umeme cha Ibadakuli Shinyanga utasaidia kupunguza adha ya kukatika kwa umeme katika mikoa ya kanda ya ziwa...
Hayo ameyasema leo 13,3,2026 wakati akielezea maendeleo ya mradi huo kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea Mkoani Shinyanga, ambapo amesema mradi huo utakamilika October mwaka huu.
Ndejembi amesema mradi huu ukikamilika utanufaisha wananchi na kuondokana na changamoto ya kukatika katika kwa umeme, hivyo watu watafanya kazi zao bila usumbufu wa kukosa nishati hiyo kwa sababu serikali inafanya hivi ili kuongeza uhakika wa umeme.
Ndejembi amesema mradi huo ulianza kujengwa mwaka 2023 una awamu mbili awamu ya kwanza ya Megawati 50 tayari imekamilika na imeanza kuingiza umeme kwenye Gridi ya Taifa na awamu ya pili itahusisha uzalishaji wa Megawati 100 zaidi na kufanya jumla ya Megawati 150 kutoka katika mradi huo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati Subira Mgallu ameipongeza serikali kwa kuongeza uhakika wa umeme ambao utasaidia kuondoa changamoto mbalimbali kwa wananchi zinazosababishwa na umeme.
"Pia tuipongeze serikali yetu kuleta mradi huu ambao utawasaidia wananchi kufanya miradi mbalimbali na kujikwamua kimaisha,pia tuishukuru wizara ya Nishati kwa kuendelea kusimamia kikamilifu"amesema Mgallu.
"Naomba niwapongeze shirika la umeme Tanzaia TANESCO kwa kusimamia na kutekeleza vizuri mradi huu wa Uzalishaji Umeme kwa nguvu ya Jua"amesema Mgallu.
Ziara ya kamati ya kudumu ya bunge nishati na madini imefika mkoani Shinyanga ikiwa ni muendelezo wa kukagua miradi mbalimbali ya Nishati, ikiwa ni pamoja na kutembelea mradi wa uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya jua ulioko wilayani Kishapu

Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi akizungumza

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati Subira Mgallu akizungumza








