
Na Suzy Butondo , Shinyanga,...BUTONDO DIGITAL
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Shinyanga wanatarajia kuzindua utalii wa ikolojia katika hifadhi ya Msitu wa Lubaga maarufu Harsh ifikapo Julai mwaka huu.
Utalii huo utahusisha shughuli mbalimbali ikiwamo kupiga picha, kupumzika pamoja na kufanyika kwa hafla kama harusi na sherehe nyingine.
Afisa mwandamizi wa uhifadhi kutoka TFS wilaya ya Shinyanga Fabian Balele akizungumza na waandishi wa habari leo Marchi 20,2026 katika hifadhi hiyo, amesema maandalizi ya kuanzisha huduma hizo yanaendelea kufanyika.
Balele amesema hifadhi hiyo ina vivutio vya asili vinavyovutia utalii wa ikolojia, hivyo wameanza kuweka miundombinu ya msingi kwa ajili ya shughuli hizo.
“Katika hifadhi hii kutakuwa na utalii wa ikolojia ukiwamo kupiga picha, kupumzika na kumbi za mikutano ya nje kwa ajili ya hafla mbalimbali zikiwamo harusi.
Pia amesema kutakuwa na njia ya kuendesha baiskeli yenye urefu wa kilomita saba, na tunatarajia kuanzisha bustani ya wanyama,” amesema Balele.
Ameeleza kuwa watalii watakaotembelea eneo hilo watapatiwa elimu ya uhifadhi wa misitu na ufugaji nyuki ili kusaidia kulinda mazingira
"Pia tunakaribisha watu ambao watapenda kujifunza ugaji nyuki mafunzo ni bure kabisa karibuni"amesema Balele
Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka TFS Wilaya ya Shinyanga Fabian Balele akizungumza.
Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka TFS Wilaya ya Shinyanga Fabian Balele akizungumza.