BANDORA AWATOA HOFU WAFANYABIASHARA WANAOPISHA MRADI WA SOKO . | BUTONDO DIGITAL

Sunday, July 26, 2026

BANDORA AWATOA HOFU WAFANYABIASHARA WANAOPISHA MRADI WA SOKO .

  Suzy Butondo       Sunday, July 26, 2026

 


Na mwandishi wetu Tabora

Diwani wa Kata ya Chemchem wilaya ya Tabora na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora (TMC), Bandora Salum Mirambo, amewataka wafanyabiashara waliosalia katika Mtaa wa Matola, Barabara ya Salimini, kupisha ujenzi wa Mradi wa Soko Kuu la Tabora unaoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, Bandora amesema eneo hilo si rasmi kwa shughuli za biashara, hivyo ni muhimu kupisha ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati. 

Aidha, amewatoa hofu kuhusu ombi lao la kupatiwa eneo la muda la kufanyia biashara, akieleza kuwa mamlaka husika zinaendelea kulifanyia kazi.
Kwa upande wao, wafanyabiashara wameeleza kuunga mkono ujenzi wa soko hilo na kuomba utekelezaji wake uharakishwe ili waweze kurejea kuendelea na shughuli zao za biashara zinazowaingizia kipato.

Katika hatua nyingine, Bandora amewasisitiza wafanyabiashara kuzingatia usafi wa mazingira na kulipa ushuru kwa wakati. Pia amewataka kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu viashiria vyovyote vinavyokiuka utaratibu, ikiwemo watu wanaoingiza bidhaa kwa njia za magendo ili kukwepa kulipa ushuru.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wafanyabiashara, wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na Diwani wa Kata ya Ipuli, Moro Juma Moro.


logoblog
Previous
« Prev Post