TAKUKURU SHINYANGA YAREJESHA ZAIDI YA SH MILIONI 21 KUPITIA UFUATILIAJI WA MIRADI | BUTONDO DIGITAL

Friday, May 29, 2026

TAKUKURU SHINYANGA YAREJESHA ZAIDI YA SH MILIONI 21 KUPITIA UFUATILIAJI WA MIRADI

  Suzy Butondo       Friday, May 29, 2026

 


Na Suzy Butondo, Shinyanga

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kurejesha zaidi ya shilingi milioni 21 kupitia ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, uchunguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa elimu kwa umma.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi 2026, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy, amesema  kati ya fedha hizo sh milioni 
 5,540, 254    zimeokolewa kupitia ufuatiliaji wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya awali na Msingi Tinde B iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Baada ya kubainika kuwa sh 5,316,304 ambazo zilipaswa kulipwa katika mamlaka ya mapato (TRA) ikiwa ni kodi ya zuio na Sh   223,950 ikiwa ni ushuru.

Pia amesema kati ya kiasi hicho sh milioni 9,672,000 zimeokolewa kupitia uelimishaji kwa njia ya semina iliyotolewa kwa viongozi wa vyama vya msingi vya kilimo vya kilimo na masoko (AMCOS) vya wilaya ya Kishapu ambavyo vinadaiwa na makampuni  ya ununuzi wa zao la pamba.

Aidha TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo 19 yenye thamani ya sh 3,906,564,882. atika sekta za elimu, afya miundombinu na maji.

Kessy amesema pia kuwa TAKUKURU iliendesha semina kwa viongozi wa Vyama vya Msingi vya Kilimo na Masoko (AMCOS) Wilaya ya Kishapu, hatua iliyosaidia kuongeza uelewa kuhusu namna ya kufuatilia madai yao dhidi ya baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao la pamba.

Ameeleza kuwa katika juhudi za kuzuia rushwa, taasisi hiyo ilifanya ufuatiliaji wa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan mradi wa ujenzi wa shule hiyo, na kubaini kuwa fedha hazikuwa zimelipwa kama ilivyostahili.

“Kupitia mapendekezo yaliyotolewa na ufuatiliaji uliofanywa, fedha zote zililipwa katika mamlaka husika,” amesema Kessy.

Aidha Kessy ametoa wito kwa taasisi zote za umma kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya maadili, pia wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga amewaomba kushirikiana kikamilifu na TAKUKURU katika juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii kwa ujenzi wa jamii.

Fedha zingine zimeokolewa kutoka sekta mbalimbali baada ya Takukuru Shinyanga kufanya uchunguzi wake kwa kina.

"Wananchi wote niwaombe mkipata taarifa yeyote inayoashiria rushwa mtoe taarifa kupitia namba 113 bure kwani kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu, hivyo niwaombe tutimize wajibu wetu"amesema Kessy



logoblog
Previous
« Prev Post