WATUHUMIWA 35 WANASWA SHINYANGA, POLISI WAPIGA VITA WIZI WA VIFAA YA SGR NA UZEMBE BARABARANI | BUTONDO DIGITAL

Saturday, April 4, 2026

WATUHUMIWA 35 WANASWA SHINYANGA, POLISI WAPIGA VITA WIZI WA VIFAA YA SGR NA UZEMBE BARABARANI

  Suzy Butondo       Saturday, April 4, 2026

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomiakitoa taarifa kwa waandishi wa habari Shinyanga


Suzy Butondo, Shinyanga
BUTONDO DIGITAL

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata watuhumiwa 35 pamoja na vielelezo 306 vya aina mbalimbali, vikiwemo vinavyohusiana na mradi wa ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR), katika halmashauri za Msalala na Shinyanga.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni iliyofanyika kuanzia Machi 1 hadi Machi 31 mwaka huu. Amebainisha kuwa kati ya watuhumiwa hao, nane wanahusishwa na wizi wa vifaa vya mradi wa SGR.

Magomi amesema kuwa watuhumiwa wote walikamatwa wakiwa na vielelezo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vipande 306 vya nondo, mabomba 32 yenye ukubwa wa milimita 12, stendi 12 za makarasha, pamoja na mabomba ya mraba (square pipes) 65.

Kwa upande wa Kikosi cha Usalama Barabarani, jeshi hilo limeendelea na operesheni dhidi ya madereva wasiotii sheria za barabarani. Katika operesheni hizo, madereva watatu wamefungiwa leseni zao kwa kipindi cha miezi mitatu kila mmoja, kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo unaozidi kilomita 80 kwa saa (80 KPH).

Aidha, jumla ya makosa 5,648 yamekamatwa, ambapo makosa ya magari ni 4,044 ya bajaji pamoja na pikipiki ni 1,604. Wahusika wote walichukuliwa hatua kwa kulipa faini za papo kwa papo.

Kamanda Magomi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Pia amewakumbusha wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka.
logoblog
Previous
« Prev Post