TABORA: Klabu ya Rhino Rangers yenye maskani yake mkoani Tabora imeendelea na maandalizi yake kupitia mazoezi makali kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Stand United, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi, Oktoba 3, 2026, majira ya saa 10:00 jioni katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Katika maandalizi hayo, uongozi wa klabu umeendelea kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuipa timu sapoti katika michezo yake ijayo, hatua inayolenga kuongeza morali na kujiamini kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Makamu Mwenyekiti wa Rhino Rangers, Bandora Salum Mirambo, amewataka mashabiki kuendelea kuwa pamoja na timu hiyo, akisisitiza kuwa uwepo wao uwanjani na sapoti wanayoitoa ni sehemu muhimu katika kuipa timu nguvu ya kupambana na kutafuta matokeo mazuri.
Bandora amesema kuwa mashabiki wanapokuwa mstari wa mbele kuiunga mkono timu, wachezaji hupata hamasa zaidi ya kujituma na kupambana ndani ya uwanja.
Sasa macho ya “Faru” yanaelekezwa Shinyanga, ambapo Rhino Rangers inatarajiwa kukutana na Stand United katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kituo kinachofuata ni Shinyanga!
🐘 RHINO RANGERS — “Safari yetu ya ushindi inaendelea.”
